|
Pamba ya Mkulima Haitochukuliwa kwa Mkopo- Mkuu wa Mkoa wa Tabora Serikali ya Mkoa wa Tabora imesema kuwa malipo kwa ajili zao la pamba yatatolewa papo kwa hapo mkulima anapouza mazao yake katika Kampuni zilizopangiwa kununua zao hilo mkoani Tabora.Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa kuhamasisha mbinu bora za ulimaji wa zao la pamba katika Halmashauri ya wilaya ya Urambo. Alisema kuwa utaratibu utakaotumika katika uuzaji na ununuzi wa pamba mkoani Tabora ni wa nipe nikupe na kusisitiza hakutakuwa na utaratibu wa njoo wiki ijayo au kesho. Mwanri alizitaka Kampuni zote zilizopangiwa kununua pamba zikafanya maandilizi ya kutosha ili kuepusha usumbufu kwa wakulima kwa kukopa mazao yao. |
Alisema kuwa utaratibu wa kukopa mazao ya wakulima ndio umekuwa ukisababisha wakate tamaa na kusababisha uzalishaji wa zao hilo kudhofika, lakini wakilipwa palepale wakulima watapata hamasa na kulima kwa wingi zaidi katika msimu unaofuata.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alitoa wito kwa wakulima waliojitokeza kulima zao hilo kuzingatia kanuni na sheria zakilimo cha zaoa la pamab kwa kuepuka kuweka uchafu na kumwagia maji pamba yao iliwaweze kupata bei nzuri. Alisema kuwa mtu atakayebainika kuchafua pamba kwa lengo la kufanya udanganyifu atachukuliwa hatua kalikulingana na sheria inayoongoza zao hilo. Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa huyo amesisitiza Kampuni zote zinazosambaza pembejeo kwa wakulima wa pamba kuhakikisha pembejeo hizo zinawafikisha wakulima kabla ya mwisho wa wiki ijayo ili waweze kwenda sanjari na msimu wa kilimo. Alisema kuwa zaidi ya hapo watasababisha wakulima washindwe kuzalisha kwa wingi na kupata mafanikio kidogo. Naye Mweneyekiti wa Halamshauri ambae pia ni diwani wa Kata ya Uyumbu Mhe Adam H. Malunkwi alisema kuwa kuliibua tena zao la pamba kutawasaidia wakazi wa Halamashauri ya wilaya ya Urambo kwani ununuzi wa zao la Tumbaku limekuwa likisuasua kwa misimu iliyopita. Aidha, Mhe. Adam aliomba mbegu ziwahi kufikakatika maeneo yote ambayo wakulima wamejiandikisha kwa ajili ya kulima zao hilo na kuongeza kuwa watazingatia elimu iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa ili waweze kuzalisha kilo 1000 hadi 1200 katika ekari moja. MWISHO |
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.