Kamishina Mhe. Elibariki Bajuta Mkuu wa wilaya Urambo akiambatana na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji(W) Urambo na baadhi ya Wataalamu leo Jumanne ya Novemba 7, 2023 amefanya ziara kata ya Kasisi kijiji cha Wema na kukagua ujenzi wa Zahani ya Wema na kulizishwa na hatua ya ujenzi huo.
Wakati akiwasalimia wanachi wa kijiji cha Wema, Mhe. Macho S. Ntayega Diwani Kata ya Kasisi amesema fedha zilizotumika ni Tsh milioni 68,520,000 ikiwemo Tsh milioni 7,800,000 michango ya wananchi, Tsh 720,000 mchango wa Halmashauri na Tsh milioni 60,000,000 ni fedha kutoka Serikali Kuu na wamekamilisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), vyoo vya wanawake na wanaume, kichomea taka pamoja na kujenga shimo la kuhifadhi kondo la nyuma.
Mhe. Bajuta amewapongeza wananchi wa kijiji cha Wema, Serikali ya kijiji na Mhe. Diwani wa kata ya hiyo kwa uaminifu, uadilifu na kuwa mfano kwa kukamilisha ujenzi uliozingatia ramani ya wizara, majengo yenye ubora na viwango vinavyotakiwa hivyo kuakisi thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali.
Mhe. Bajuta amesema " mimi binafsi hapa nimelizika na hatua ya ujenzi na wananchi hawa wanahitaji huduma siyo kuangalia haya majengo, wiki ijayo nilikuwa na safari lakini nimewiwa kuunga mkono juhudi zenu nimehairisha safari nitarudi hapa kufungua hii zahanati ili wananchi hawa wapate huduma kwanza"
Pamoja na pongezi hizo, Mhe. Bajuta ameitaka jamii ya kijiji cha Wema kutambua ya kuwa zahanati hiyo ni mali yao hivyo hawana budi kuilinda miundombinu iliyopo, majengo pamoja na vifaa tiba vilivyopo kwa maslahi yao na Taifa.
Pia mhe. Bajuta amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji(W) kuhakikisha mipaka ya zahani hiyo inatambuliwa na kuwekewa alama ili pasiwepo na migogoro ya uvamizi wa eneo la zahanati.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.