Tarehe 8. Machi ya kila mwaka ni sikukuu ya Wanawake wote Duniani, na katika kuhazimisha sherehe hizo zilizofanyikia katika ukumbi wa Halmashuri ya Wilaya ya Urambo, Mkuu wa Wilaya Mhe. Angelina Kwingwa ametoa ujumbe na kauli mbiu ya Kitaifa inayosema "Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Tuimarishe usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake wa Vijijini" na ametumia fulsa hiyo kuwaasa akina mama kuwekeza katika viwanda vya Kati.
Mhe. Kwingwa amewataka akina mama kujishughulisha na kujipanga katika uwekezaji hasa wa viwanda vya kati. “Weka malengo ya mbele kwa kila shughuli ya uzalishaji unayoifanye na kujenga misingai imara katika biashara unayoifanya itayokuwezesha kusonga mbele ” amesema hayo Mhe. Kwinga.
Mhe. Kwinga alisisitiza ya kuwa wanawake wazitafute fulsa na wasitegemee kuwa ipo siku fulsa zitawatafuta wao, pia aliwakumbusha kurejesha mikopo ya taasisi mbalimbali ili kujenga uhaminifu wa kukopesheka zaidi.
Awali akisoma lisala ya akina mama mbele ya mgeni rasmi, Bi Elizabeth Kaholwe afisa maendeleo ya jamii alionyesha umuhimu wa mwanamke katika jamii katika shughuli za uzalishaji, malezi ya watoto na mahitaji ya familia kwa ujumla.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.