Na Edward C. Rumanyika
Akionekana mwenye bashasha na uso wa furaha, Balozi Dk. Batrida Buliani Mkuu wa Mkoa wa Tabora amewapongeza viongzi wa Wilaya ya Urambo akiwemo Mhe. Magret Simwanza Sitta(MB), Mkuu wa wilaya, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Mhe. Adam Malunkwi (Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani), Baraka Zikatimu (Mkurugenzi Mtendaji), wahe. Madiwani na watendji waandamizi wa Halmashuri kwa ushirikiano mkubwa unaonekana katika swala zima la kuwahudumia wananchi, kusimamia ujenzi , ukamishilishaji wa miradi ya maendeleo na ukusunyaji wa mapato ambapo hadi kufikia Juni 23, 2022 makusanyo yalifikia 94%.
Balozi Dk. Buliani akiwa anahutubia Baraza Maalum la wahe. Madiwani la hoja za Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Juni 24, 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Urambo kwa mwaka unaoishia Juni 30, 2021 imepata Hati Safi yaani Unqualified Opinion amesema hana wasiwasi na Urambo ya sasa maana kuna mabadiliko makubwa sana ya utendaji kazi hasa kwenu viongozi mliochaguliwa, na wateule wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwaomba waendelee kutekeleza ilani ya CCM kwa mshikamano wa pamoja walionao, kuwasimamia Timu ya Watalaam wa Halmashauri (CMT) ili kuhakikisha kero za wananchi zinatatuliwa kwa wakati.
"Urambo mna ubunifu, na niwaombe mtoke mjifunze zaidi ikibidi mwende hata Mkoa wa jirani wa Katavi kuna kitu kitawaongezea tija zaidi, Mkurugenzi ni mbunifu amefika hapa ndani ya muda mfupi amebuni vyanzo vipya vya mapato na kwenye mkoa yeye anaongoza kwenye usimikaji na utumiaji wa mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji wa mapato maana katika vituo vya afya 27 vya kutolea huduma yeye kafunga mfumo wa GoT-HoMIS vituo 23 na hivyo vituo 4 amesema vifaa vipo ila kuna changamoto ya umeme hongereni sana Mkurugenzi", alisema Balozi Dk. Buliani.
Awali Balozi Dk. Buliani aligusia ajari ya Treni ya abilia iliyotokea mkoani Tabora Juni 22, 2022 na kusema abilia wote wamesafirishwa na majeruhi wanaendelea na matibabu katika hospitali mbalimbali hapa nchini, ingawa taarifa ya awali iyotolewa kwenye vyombo vya habari ilisema kulikuwa na vifo 4 ukweli ni kwamba baada ya kunyanyua mabehewa yote idadi ya vifo ni 3 maana kuna sehemu ya kichwa ilikatika na kuhesabiwa kama mwili na wakahisi mwili upo chini ya mabehewa kumbe ilikuwa ni sehemu ya mwili mmoja uliokuwa umesagika kwa kukanyagwa na Treni, lakini kwa yote tuzidi kuwaombea majeruhi wapone haraka na kuendelea kulitumikia taifa.
Katika kuhitimisha hotuba yake Balozi Dk. Buliani ameitaka Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango kuhakikisha inasimamia Kamati ya Wataalam ya Halmashauri (CMT) inaleta utekelezaji wa hoja zote zilizoibuliwa na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2020-2021 na miaka ya nyuma (previous) kwenye vikao vya Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango vya kila robo mwaka. Pia hoja zinazo stahili kuombewa kibali cha kufutwa kwa mujibu wa Waraka namba 1 wa Ofisi ya Waziri Mkuu wa Mwaka 2015 utaratibu ufuatwe ili ziweze kufutwa.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.