Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia Pro. Joyce Lazalo Ndalichako(Mb) amezindua Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha wilaya ya Urambo (VETA Urambo) katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyikia katika viwanja vya Chekeleni kata ya Ussoke Jumanne ya 09.07.2019 wilayani Urambo. Kwa sasa VETA Urambo chenye uwezo wa kudahili wanafunzi 160 kitatoa mafunzo ya ufundi stadi kwa kozi ndefu kwa kipindi cha mwaka 1 katika fani 4 za Ushonaji wa Nguo(Tailoring), Umeme wa Majumbani (Domestic Electrical Installation -DEI), Uashi(Masonry and Bricklaying -MB) na Uhazili na Kompyuta (Secretarial and Computer SC) na mafunzo haya yanaanbatana na masomo ya Hesabu, Engineering Science, Kingereza, Michoro, Ujasiliamali, Stadi za Maisha na Usalama kazini.
Akihutubia umati wa wananchi, viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa VETA kanda ya Magharibi, Prof.Ndalichako amesema Serikali ya awamu ya Tano imejipanga kuhakikisha kila wilaya nchini inakuwa na Chuo cha Elimu na Mafunzo ili kuwezesha watanazania kupata ujuzi wa fani mbalimbali ili waweze kujiajili na kuajiliwa katika vianda vinavyoendelea kujendwa nchini kwa kadri ya mahitaji ya soko la ajira.
Pia Prof. Ndalichako ameutaka uongozi wa wilaya ya Urambo na viongozi wa VETA Urambo kuhakikisha raslimali yakiwemo Majengo, miundombinu mingine inayotarajiwa kujengwa pamoja na mipaka ya chuo kutunzwa na kulindwa vizuri wakati Serikali ikijiandaa kutuma timu ya wataalamu kuja kufanya tathmini ya ujenzi wa Bwalo la chakula, Karakana ya Ufundi wa Magari(motor vehicle mechanics), Madarasa ya Uungaji wa Vyuma (welding and Fabrication), Ufundi Bomba, Ukarimu wa Holeti (Hotel Management), Ukumbi Mkubwa na Mabweni ya Wanafunzi.
Awali Mhe. Magreti Simwanza Sitta(Mb) Jimbo la Urambo wakati wa kusalimi wananchi na kutoa shukrani kwa mgeni rasmi prof. Ndalichako, amewasihi wananchi wote wa Urambo kutumia fursa hii ya kipekee ya Chuo cha Ufundi Stadi VETA Urambo kuleta watoto wao hasa wa kike kujifunza fani mbalimbali zitakazotolewa na VETA Urambo. Kwa unyenyekevu Mhe. Sitta amewaomba watendaji wa Vijiji, wenyeviti wa Vijiji vyote 62 vya Urambo kutambua watoto wenye uhitaji wa kujiendeleza katika fani za VETA Urambo na kutoa ahadi ya kugharamia kiasi cha Tsh 60,000/= kwa mwanafunzi mmoja atayesoma VETA Urambo kutoka kila kijiji cha Urambo.
Akitoa ufafanuzi zaidi Ndg. Eliya Ndiwu mkuu wa chuo cha VETA Urambo ameomba wananchi wa Urambo, mkoa wa Tabora na kote nchini kuleta watoto wao katika chuo hii kwani walimu wabobezi wakutosha wapo, madarasa ya kisasa yenye vifaa vya kujifunza na kufundishia pia vinapatikana chuoni hivi sasa. Ndg. Ndiwu ameleza sifa za kujiunga kuwa ni elimu ya darasa la saba na kuendelea isipokuwa kwa fani Uhazili na Kompyuta elimu ni kidato cha 4, na upatikanaji wa fomu ni katika vyuo vyote vya VETA nchini kuanzia tarehe 10.07.2019 hadi 25.07.2019. Pia ametoa mawasiliano ya chuo cha VETA Urambo kuwa ni VETA Urambo Box 1218 Tabora simu +255 787 682 697 na +255 765 765 790 na barua pepe ya vetawesternzone@veta.go.tz
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.