Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kushoto pichani apo juu), akizungumza na waandishi wa Habari Kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari-Bunge mjini Dodoma kuhusu hatua ya Serikali ya kuanza kulipa madeni ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa Umma, kiasi cha shilingi bilioni 43.39 kuanzia Februari 10, 2018.
|
MAELEZO YA MHE. DKT. PHILIP ISDOR MPANGO KWENYE VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MALIPO YA MADAI YA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA
Ndugu Wawakilishi wa vyombo vya habari, nimewaiteni leo hii ili niwape taarifa fupi kuhusu malipo ya madai ya malimbikizo ya mishahara kwa
Watumimishi wa umma waliokuwa na madai ili muweze kuufikishia umma wa Watanzania.
Serikali kupitia mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara (Human Capital Management Information System – HCMIS/Lawson) kufikia tarehe 01 Julai 2017 ilikuwa na madai ya malimbikizo ya mishahara yenye jumla ya shilingi 127,605,128,872.81 kwa watumishi 82,111 Wakiwemo walimu 53,925 waliokuwa wanadai shilingi 53,940,514,677.23 sawa na asilimia 42.27 ya madai yote, na wasiokuwa walimu 28,186 waliokuwa wanadai jumla ya shilingi 73,664,614,195.58 sawa na asilimia 57.73 ya madai yote. Madai haya yalikuwa ya muda mrefu mengine yakiwa ya kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2017.
Madai haya yalijumuisha mishahara isiyolipwa, tofauti ya mishahara kutokana na kukaimu na nyongeza za mishahara zilizotokana na kupandishwa vyeo na kuchelewa kurekebishiwa mishahara.
Madai ya watumishi 27,389 kati 82,111 yenye jumla ya shilingi 43,393,976,807.23 ikiwa ni asilimia 34 ya madai yote ya shilingi bilioni 127,605,128,872.81 yaliyohakikiwa yameonekana ni sahihi na yanastahili kulipwa bila marekebisho.
Pakua Majina yao Katika ngazi ya Kitaifa, Kimkoa na Kiwilaya apo chini
Majina yao Kitaifa
|
Majina yao Kimkoa-Tabora
|
Majina yao Kiwilaya-Urambo
|
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.