Siku ya Mtoto Afrika 16.06 2023 Songambele Urambo kauli mbiu ni Zingatia Usalama wa Mtoto katika Ulimwengu wa Kidigitali
Mhe. Kenani Kihongosi Mkuu wa wilaya ya Urambo ameiomba Jamii ya Wana Urambo kushirikiana kuhakikisha Maadili na Malezi ya mtoto inakuwa Kipaumbele chetu kwa ajili ya kuandaa Kizazi chenye Maadili kama Taifa la Kesho.
Mhe. Kihongosi ameyasema hayo hii leo wakati akihutubia sherehe za mtoto wa Afrika leo 16 Juni, 2023 katani Songambele sherehe zilizoambatana na jumbe mbalimbali zilizoelezea wajibu wa mzazi, mlezi anatakiwa kufanya nini katika malezi ya mtoto, pia ujumbe kwa watoto wenyewe wazingatie vitu gani katika makuzi yao.
Mhe. Kihongosi amewapongeza akina mama wa wilaya ya Urambo wakiongozwa na Mhe. Margaret Sitta Mbunge wa Jimbo la Urambo kwa malezi mazuri na ya Kimaadili na kufanya hivyo wanaliadaa Taifa imara na lenye Maadili, aidha amewapongeza akina baba wote kwa kujitoa kwa dhati kuhakikisha familia zao zinapata mahitati yote ya msingi ya kila siku.
Mhe. Kihongosi amesisitiza wazazi wa Urambo kuachana na malezi ya kisasa na kushindwa kusimamia wajibu wao kama wazazi hasa tabia za kuwapatia simu janja watoto na watoto kuona vitu visivyofaa kuonwa na watoto na kusema "simu tunawapa sisi, na wanayoyaona wanaiga mwisho wake wataishia kulelewa na polisi na magereza zetu".
Akihitimisha hotuba yake, Mhe. Kihongosi amewaomba viongozi wa Vyama, Serikali, Dini na Jamii kukemea kwa nguvu tabia ya Ushoga na Usagaji na kuwataka maneno hayo yatajwe kama yalivyo ili yaeleweke kwa watoto na siyo kutafuta maneno mengine yanayojaribu kuficha ubaya wa uovu huo.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.