Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Paul Chacha amewataka Wananchi wa Tabora kutunza Mazingira kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Mhe. Paul Matiko Chacha amesema hayo wakati akihutubia katika maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani ambapo Kimkoa yamefanyika katika Wilaya ya Urambo tarehe 05.06.2025 huku akisisitiza uendelevu wa uhifadhi wa mazingira Wilayani Urambo. Pia amezielekeza Mamlaka zinazohusika kusimamia Mazingira, kuelimisha jamii za wakulima na wafugaji zinazotajwa kuharibu mazingira kutokana na shughuli zao za ufugaji na kilimo cha tumbaku.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya kaliua Ndg. Raymond Mweli amesema kuwa, watayaishi maelekezo ya Serikali katika kuhakikisha usalama wa mazingira unazingatiwa katika maeneo yao, wakiamini kwamba kuishi katika mazingira safi kunasaidia kuondokana na maradhi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bi. Grace Quintine amesema kuwa, lengo la Halmashauri na Mipango kuhusu Mazingira, ni kuweza kuendeleza yale yanayofanyika ya Kufanya usafi mara kwa mara kama ambavyo leo Watumishi na Wananchi Wa Urambo walipoungana kufanya usafi.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe. Margaret Sitta amesema jamii ikielimishwa umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji kutokata miti na kupanda miti kutasaidia kuondokana na changamoto zitokanazo na uharibifu wa mazingira ikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi.
Mhe Paul Chacha katika maadhimisho ya Siku hii ya Mazingira amewaongoza Wananchi wa Urambo katika zoezi la usafi wa mazingira katika stendi kuu ya Mabasi pamoja na kupanda miti, ikiwa ni ishara ya kuendelea kuthamini mazingira na kuadhimisha siku hii muhimu.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.