Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bi. Grace Quintine, katika tafrija ya kuwapokea na kuwapongeza wanafunzi walioshiriki michezo ya UMISSETA 2025 Mkoani Tabora.
Tafrija hiyo imefanyika katika Bwalo la Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Margeret Sitta mnamo tarehe 07.06.2025 baada ya wanafunzi hao kuwasili wakitokea Manispaa ya Tabora yalipofanyika mashindano hayo.
Katika mashindano hayo Timu ya wanafunzi kutoka Urambo DC imeweza kubeba vikombe katika mchanganuo ufuatao.
1. Mpira wa Miguu Wavulana nafasi ya kwanza.
2. Mpira wa Miguu Wasichana nafasi ya Tatu.
3. Mpira wa Wavu ( Volleyball) Wavulana nafasi ya Pili
4. Mpira wa Wavu (Volleyball) Wasichana nafasi ya pili.
5. Mpira wa kikapu Wavulana nafasi ya pili.
6. Mpira wa Mikono (Hand ball) Wavulana nafasi ya tatu.
7. Mpira wa Meza (Table Tenis) Wavulana nafasi Ya Pili.
8. Mpira wa Meza (table Tenis) Wasichana nafasi ya kwanza.
9. Mpira wa goli Wasichana nafasi ya pili.
10. Riadha maalumu nafasi ya kwanza.
11. Nidhamu na hamasa nafasi ya kwanza.
Wilaya ya Urambo imetoa Wanamichezo....kuunda Timu ya Mkoa kwenda kushiriki kwenye Mashindano yanayoendelea kwa sasa Mkoani Iringa ambako Kitaifa Yanafanyikia Iringa.
Aidha Mkurugenzi Quintine alieleza kuwa ni mara yake ya kwanza kushinda mchezo pendwa wa Mpira wa Miguu Wavulana, hivyo amewapongeza sana wanafunzi hao.
Sambamba na hilo ameelekeza Divisheni ya Elimu kuweza kuweka mazingira vizuri mapema kwa kushirikiana na Kitengo cha Utamaduni, Sanaa na Michezo katika mashindano yajayo kwa mwaka 2026, kwani maandalizi yakiwa mazuri yatasaidia timu kufanya vizuri katika mashindano hayo.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.