Maandamano ya wanafunzi shule za msing 77 na sekondari 17 Wilyani Urambo yamefanyika leo tarehe 02.07.2018 ikiwa ni siku ya kufungua shule Muhula wa Pili Kitaifa kuanzia saa 1:30 Asubuhi hadi saa 5:00 Asubuhi na kupokelewa na Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Urambo Bi Angelina John Kwingwa katika viwanja vya Mwananchi Square lengo ikiwa ni kupinga utoro shuleni, Ndoa na Mimba za Utotoni, utumikishwaji katika mashamba ya Tumbaku, Migodini, Kazi za Ndani na Biashara Ndogondogo.
Wanafunzi wapatao 9358 wa shule za msingi Azimio, Mabatini, Mwenge, Urambo,Ukombozi, Imalamakoye, Umoja na Tulieni na wanafunzi 2150 wa shule za sekondari Urambom day, Chetu na Ukombozi zote za Umma zilizopo katika tarafa ya Urambo wameandamana wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali za kuonyesha kudai haki yao ya msing ya elimu, huku wakisindikizwa na walimu wao wapatao 276, (Msingi 206 na Sekondari 70). Maandamano haya pia yamefanyika kila kata na kupokelewa na wahe. Madiwani na viongozi mbambali wa serikali za Kata na Vijiji.
Akihutubia waandamanaji, wazazi wa wanafunzi, watumishi wa Tarafa ya Urambo na wananchi wengine waliohudhulia katika viwanja vya Mwananchi Square, Bi Angelina Kwinga ameeleza fedhea iliyoukumba Mkoa wa Tabora Aprili 2, 2018 Mkoani Geita siku ya ufunguzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ambapo Mkoa wa Tabora ulitwaja kuwa miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa Utoro shuleni.
Bi Kwinga amewataka wazazi, walezi kujenga utamaduni wa kutembelea shule na kuwa wepesi wa kufatilia mahudhulio ya darasani na tabia za watoto wao, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya kitaaluma kupitia walimu wao. Ameiomba jamii inayomzunguka mwanafunzi, Viongozi wa Serikali ngazi zote ikiwemo viongozi wa madhehebu ya dini kukemea kwa pamoja vitendo vinavyochangia utoro kwa wanafunzi wa shule.
"Mkuu wa Polisi -OCD, nakuagiza watakao husika na mimba za wanafunzi, ndoa za utotoni au ndoa chini ya umri husiokubalika kisheria weka ndani muoaji, muolewaji, wazazi wa pande zote mbili na aliyefungisha ndoa hiyo" amesema Bi Kwinga.
Aidha amewapongeza walimu kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwaomba wawe wavumilivu wakati Serikali inafanyia kazi changamoto za kielelimu ikiwemo miundombinu, vifaa vya kujifunza na kujifunzia na stahiki zao lakini akawasihi changamoto hizo zisiwafanye wakawa watoro kazini.
Awali akitoa takwimu za utoro shuleni kwa mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji (W) Ndg Osear Mwambusira amewaagiza walimu wakuu na wakuu wa shule kuwapokea watoto wote watoro watakaoonekana kuitikia agizo la serikali la kurudi shuleni ili waendelelee na masomo na taarifa ya watakao kaidi ipatikane mapema haraka iwezekanavyo ili wasakwe popote walipo na sheria ichukue mkondo wake.
Akizungumza kwa niaba ya wazazi, walezi na jamii Bi Agness Ndinya Kulwa ambae pia ni Mwalimu mzoefu katika shule ya msingi Mwenge amekili kuwepo kwa tatizo la utoro shuleni na akaeleza sababu ni kutokana na mwamko mdogo wa wazazi kuhusu Elimu, na akasema wengi wa wazazi wanatumia watoto wao kuwa kama sehemu ya walezi wa familia hizo kuwa kuwatuma na kuwaagiza kuuza bidhaa hasa siku za Minada na Gulio.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.