Urambo, Tabora.
Halmashauri ya Wilaya ya Urambo imefaniwa kufanya kikao chake cha kwanza kidigitali kupitia mfumo wa e-board mnamo tarehe 15.04.2025, ikiwa ni katika kuenda sambamba na kasi ya mabadiliko ya teknolojia pamoja na utunzaji wa mazingira.
Mfumo huo wa e-board umeanza kutumika katika kikao cha kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira na kufuatiwa na kikao cha kamati ya Elimu na Afya. Vikao hivyo vimepata mafanikio makubwa kutokana na uelewa wa wajumbe juu ya matumizi ya mfumo huo wa e-board.
Hatua hii ya matumizi ya mfumo wa e-board, inaondoa matumizi ya makabrasha yaliyokuwa yakitumika awali, jambo ambalo linapunguza gharama pamoja na matumizi ya karatasi, hivyo kuenda sambamba na sera za Taifa juu ya utunzaji wa mazingira pamoja na matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika kutekeleza shughuli za Serikali.
Ikumbukwe kuwa, mnamo tarehe 31.01.2025 katika Mkutano wa Baraza la Madiwani, Madiwani wote waliweza kupatiwa vishikwambi ambavyo vilitarajiwa kutumika katika vikao mbalimbali sambamba na shughuli nyingine za Serikali.
Aidha wajumbe wa vikao hivyo vya kwanza wameipongeza Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kwa kufanikisha mabadiliko hayo jambo ambalo limesaidia sana katika kupunguza gharama za uendeshaji wa vikao pamoja na ufanisi katika uendeshaji wa vikao.
Hata hivyo, Halmashauri ya Wilaya ya Urambo itaendelea na matumizi ya mfumo huu wa e-board katika vikao vyake, ikiwa ni katika kuhakikisha lengo la Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhakikisha Taasisi zake zinatumia mifumo ya TEHAMA linafikiwa.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.