Urambo - Tabora
Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Dkt. Khamis Mkanachi amezindua zahanati ya kijiji cha Mlangale Kata ya Songambele tarehw 26.06.2025 ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kuhakikisha kila kijiji kinapata Zahanati.
Mhe. Dkt. Mkanachi katika Sherehe za Uzinduzi huo aliambatana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Mkurugenzi mtendaji akiwa na Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo.
Aidha Mhe. Dkt. Mkanachi amemshukuru Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweka kipaumbele katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora katika Sekta mbalimbali kama vile Afya, Elimu, Kilimo n.k. aliendelea kwa kusema kuwa Mpango wa Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha kuwa huduma za afya zinasogezwa karibu na wananchi. Hivyo ameeleza kuwa Zahanati ya Mlangale haitokuwa ya mwisho kuzinduliwa.
kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Urambo Bi. Grace Quntine amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa Fedha kutoka Serikali kuu kwa ahili ya ukamilishwaji wa Zahanati hiyo pamoja na miradi mingine ya Maendeleo. Aidha amempongeza na kumshukuru Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe. Margaret Sitta kwa kuendelea kuwa karibu na Halmashauri ambapo kwa zahanati ya Mlangale alitoa Mifuko 100 ya Saruji, hali iliyochangia wananchi wa kijiji cha Mlangale kufanikisha ujenzi wa Zahanati yao.
Aidha amemshukuru Mkuu wa Wilaya Mhe. Dkt. Khamis Mkanachi kwa kuwa karibu na Halmashauri katika kuongeza Nguvu kwenye Usimamizi wa Miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Urambo.
Kwa upande wake aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo Ndg. Elias Kafwenda ametoa shukrani zake za Dhati kwa Serikali kutokana na kupokea fedha kutoka Serikali kuu na Halmashauri, hali iliyopelekea maendeleo hayo kufikiwa.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.