Timu ya wanafunzi wa Shule za Sekondari walioshiriki mashindano ya UMISSETA Mkoani Tabora imeng'ara na kufanya vyema katika michezo mbalimbali na kufanikiwa kubeba jumla ya vikombe 10.
Vikombe hivyo vimekabidhiwa katika hafla ya kufunga mashindano ya UMISSETA Mkoa wa Tabora mnamo tarehe 06.06.2025, na Mgeni Rasmi Mwl. Upendo Rweyemamu.
Katika mashindano hayo yaliyofanyika Mkoani Tabora katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wavulana Tabora (Tabora Boys), Timu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Urambo pamoja na Kuwa Mshindi wa Kwanza katika mchezo wa Mpira wa Miguu, timu hii iliweza kushinda michezo mingine katika nafasi za kwanza, pili na tatu.
Aidha katika Vikombe hivyo, timu iliweza kushika nafasi ya kwanza katika kipengele cha Nidhamu na Hamasa, hii imedhihirisha kuwa timu ilishika na kuyaishi maelekezo yaliyotolewa katika tafrija ya kuiaga timu ilipokuwa ikielekea Mkoani Tabora mnamo tarehe 31.05.2025, ambapo Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji Bw. Masudi aliwasihi kuwa na nidhamu na kuishika kwani ndiyo njia ya mafanikio.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.