Ofisi ya TANROAD Mkoa wa Tabora imezurudisha jumla ya nyumba 13, ofisi 1 na chumba 1 cha maabara kuwa miliki ya Halmashauri ya wilaya ya Urambo kuanzia tarehe 5.6 2018, kwa makabidhiano maalumu yaliyofanyikia katika viwanja vya Chekeleni kijiji cha Sipungu mbele ya Mhakiki Msaidizi wa Mali za Serikali Ndg Edward Laswai. Akikabidhi kwa niaba ya meneja TANROAD Mkoa Tabora Ndg. Joseph Paul Mkuu wa Kitengo cha Utawala na Fedha ameleza kuwa nyumba hizo zilikuwa ni za Mhandisi Mshauri wa Mradi wa Ujenzi wa barabara ya NDONO-URAMBO, ambapo tayari umekamilika hivyo nyumba hizo zinakabidhiwa kwa Halmashauri, "nyumba hizi bado ni imara, nzuri na za kisasa hivyo ana imani kuwa zitapangiwa matumizi kulingana na mahitaji ya Halmsahauri na hazitotelekezwa na kuwa magofu" alisema hayo Ndg Paul. |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mhe. Adam H. Malunkwi (Diwani kata ya Uyumbu) aliushukuru uongozi wa TANROAD Mkoa wa Tabora kwa maamuzi ya busara ya kuipatia Halamshauri ya Wilaya ya Urambo nyumba hizo na kuhaidi kuwa zitatumika kama Halamshauri ilivyoomba kupitia kwa Mhe. Margaret Sitta (MB Jimbo la Urambo )
Mkurugenzi Mtendaji(W) alimwagiza Ndg Ndele Mwampamba ambaye ni Afisa Ugavi na Manunuzi kuhakisha kuwa nyumba hizo zinafanyiwa usafi, na kuziingiza katika mali za kudumuili ziweze kutambulika kama mali za Halamshauri.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.