Urambo - Tabora.
Kamati ya Siasa Mkoa wa Tabora kupitia mwenyekiti wake Ndugu. Said Juma Nkumba, imesisitiza juu ya uelimishwaji wa wananchi juu ya umuhimu wa kutunza miundombinu ya miradi mbalimbali iliyotekelezwa kwa kiwango cha juu katika Wilaya ya Urambo.
Hayo yamesisitizwa wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa Mkoa wa Tabora iliyofanyika tarehe 16.06.2025, ambapo kamati hiyo imetembelea mradi wa maji katika Kata ya Usisya kijiji cha Sipungu, Mradi wa Shule Mpya ya Sekondari Kata ya Muungano (Tsh. Milioni 603) pamoja na Ujenzi wa Shule mpya ya Msingi katika Kata ya Kiyungi (Tsh. Milioni 364.5)
Aidha pamoja na maelejezo ya utunzaji wa miradi, Ndugu. Nkumba amepongeza ufanisi wa utekelezaji wa miradi hiyo na kusema kuwa Serikali ya awamu ya Sita imefanya kazi kubwa kwani fedha zilizoletwa zimefanya mambo mengi na makubwa kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa watanzania.
Sambamba na hilo Ndugu. Nkumba ameelekeza kuwa miradi na taasisi za Umma ziweze kupata huduma muhimu ya umeme mapema ili kuweza kufanya kazi kama ilivyokusudiwa.
Aidha Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe. Margaret Sitta amesema kuwa mafanikio yanayoonekana ni kutokana na ushirikiano anaoupata katika ngazi mbalimbali ikiwemo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Urambo pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo. Nao Waheshimiwa Madiwani wa Kata za Usisya, Muungano na Kiyungi wameshukuru Serikali kwa uletwaji wa miradi hiyo itakayosaidia jamii zao.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.