Umati wa mamia kwa maelefu ya wananchi wa kijiji cha Igunguli kata ya Uyogo wilayani Urambo leo Julai 22, 2023 wamejitokeza kwa wingi kumlaki na kumsikiliza mhe. Kenani Kihongosi Mkuu wa Wilaya ya Urambo kwa ajili ya utambulisho na uzinduzi wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari kijijini hapo, yenye jumla ya majengo 8 ya kisasa kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP).
Wakiwa na nyuso za furaha na bashasha, Wananchi wa Igunguli wametoa ahadi ya kuonesha ushirikiano wakati wote wa ujenzi wa shule hiyo mpya ya Sekondari kwa kuhakikisha wanajitoa kupitia mtaji walionao wa nguvukazi kwa kusaidia kusafisha eneo la ujenzi wa shule, kutoa ushirkiano wa kutosha kwa watalamu wasimamizi pamoja na mafundi wa mradi huo.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi wa Igunguli Ndg. Peter W. Lukinda Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Igunguli amesema, shukrani za pekee ziende kwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa kiasi cha Tsh 603,890,563 kwa ajili mradi huo mkubwa katika kijiji chao.
Mwenyewekiti huyo alisisitiza kwa kusema, "Wahe. Vingozi mlioko hapa, wananchi hawa baada ya kusikia tumeletewa mradi mkubwa walifurahi sana na katika hili wametoa eneo lote hili bure lenye takribani hekari 28 kwa ajili ya ujenzi wa mradi huu maana hatukuwa na Sekondari karibu. Sekondari ya kata iliyopo ipo zaidi ya kilometa 12 kutoka hapa kijiji cha Igunguli na viunga vyake."
Aidha, Mhe. Kenani Kihongozi Mkuu wa wilaya ya Urambo amewapongeza wananchi wazalendo wa Igunguli kwa upokeaji chanya wa mradi na kuwaomba waendeleze hali hiyo ya kizalendo kwa kuhakikisha mradi huo unakamilika kabla ya tarehe 30 Septemba, 2023 ili wanafunzi watakaofaulu mtihani wa Taifa wa darasa la saba, 2023 waweze kuchaguliwa na kujiunga na masomo Januari, 2024 katika shule hiyo.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.