Kuelekea katika Kilele cha Wiki na Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake, Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe. Margareth Sitta kwa Kushirikiana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora Mhe. Jaqueline Kainja Andrew wameongoza umati wa Wanawake wa Wilaya ya Urambo kufanya matembezi na kufanya usafi katika Hospitali ya Wilaya ya Urambo.
Matembezi hayo yaliyofanyika Leo tarehe 03.03.2025 yalianzia ilipo ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Urambo na Kuelekea katika Hospitali ya Wilaya ya Urambo ambapo walipokelewa na baadhi ya wataalamu wakiongozwa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Urambo Dkt. David Manyama.
Aidha katika tukio hilo, Mbunge wa Jimbo la Urambo alieleza kuwa ni mwanzo tu, na Siku ya kesho yaani tarehe 04.03.2025 litafanyka kongamano kubwa la Wanawake kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali.
Akizungumza na Kundi la wanawake katika hospitali ya Wilaya ya Urambo, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora Mhe. Jaqueline Andrew ameeleza kuwa, amekuwa akishirikiana na Hospitali ya Wilaya ya Urambo, na leo amekuja kwa ajili ya kuzifikisha Salamu za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha siku ya Kimataifa ya Wanawake inaadhimishwa kikamilifu.
Kwa niaba ya uongozi wa Divisheni ya Afya pamoja na Hospitali ya Wilaya ya Urambo, Mganga Mkuu Dkt. David Manyama ametoa shukrani za dhati kwa Wanawake waliojitokeza kufanya Usafi pamoja na Kuchangia damu. Ameeleza kuwa jambo hilo siyo dogo, ni jambo kubwa lenye kuleta muamko kwa jamii juu ya Mtazamo wa Mwanamke katika nyanja mbalimbali.
"Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji"
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.