Mhe. Kenani Kihongosi Mkuu wa Wilaya ya Urambo ameagiza Watendaji wa Kata 9 zilizoshindwa kufikia lengo la asilimia 100 katika afua ya kila mwanafunzi kupata anglau mlo mmoja wa chakula wakiwa shuleni kuendelea kuelimisha kuhamasisha wazazi na walezi kuchangia chakula ili watoto waweze kupata chakula wakati wa masomo na anatarajia kuona mabadiliko ya asilimia zikiongezeka wakati wa tathimini ya kikao cha robo ya kwanza kwa mwaka 2023/24.
Mhe. Kihongosi ametoa agizo hilo leo hii 27 Julai, 2023 kupitia kikao kazi cha Tathimini ya Mkataba wa Lishe robo ya nne kilichofanyika kwenye ukumbi mdogo wa mikutano wa Halmashauri na kuwasihi kila Mtendaji wa Kata kutimiza wajibu wake kwa kutumia ushawishi, maarifa na utashi aliyojaliwa na Mwenyezi Mungu kuhakikisha anaeleweka kwenye jamii kwenye uchangiaji wa chakula cha wanafunzi na siyo kutumia mabavu na nguvu kama ilivyozoeleka.
Mhe. Kihongosi amewapongeza viongozi, na wananchi wa kata 9 zinazofanya vizuri kwenye kutoa chakula kwa wanafunzi shuleni, ambazo ni kata ya Itundu, Kapilula, Kasisi, Nsenda, Ukondamoyo, Urambo, Uyogo, Uyumbu na Vumilia na kuhimiza uongozi na jamii nzima ya kata 9 zilizoshindwa kufikia lengo kutambua faida na muhimu wa kufanya hivyo ikiwa ni pamoja na kupunguza utoro na kuongeza ufaulu kwenye mitihani ya ndani na Taifa kwa ujumla. "Watendaji wetu wa Kata mliopo hapa, Wazazi/walezi waelezwe na wajue ni wajibu wao kumlea na kumdumia mtoto na kesho mtoto huyo akifanya vizuri masomoni na maisha yakaenda sawasawa atakuwa na nafasi nzuri na kubwa zaidi ya kuwahudumia wazazi/walezi wake" amesema Mhe. Kihongosi.
Awali akisoma taarifa ya Tathimini ya Mkataba wa Lishe Robo ya Nne kwa mwaka ulioishia 30 Juni, 2023, Bi Chonge Mazengo Afisa Lishe Wilaya amezitaja kata 9 zilizopata alama chini ya asilimia 76 katika afua ya kila mwanafunzi kupata anglau mlo mmoja wa chakula wakiwa shuleni ni Imalamakoye, Kiloleni, Kiyungi, Mchikichini, Muungano, Songambele, Ugalla, Usisya na Ussoke.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.