Mkutano wa wazazi wa wanafunzi wa shule Msingi za Mabatini, Azimio, Ukombozi , Mwenge, Umoja, Urambo na Tulieni zilizopo katika kata za Urambo Mjini, Mchikichini na Kiyungi umefanyika Januari 3, 2019 katika shule ya Sekondari ya Ukombozi.Wazazi hao kwa pamoja wameridhia kuchangia ukarabati wa miundombinu ya madarasa ili kuwaruhusu wanafunzi 387 wenye alama za ufauru lakini hawakuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Januari 2019.
Akihutubia katika kikao hicho Mkuu wa wilaya ya Urambo Mhe. Angelina Kwingwa amewataka wazazi hao kila mmoja kwa nafasi yake kuguswa katika kuchangia maendele ya elimu hasa hili la kuchangia uboreshaji wa miundombinu ya madarasa ili kuhakikisha wanafunzi wote wenye alama za ufaulu wanajiunga kidato cha kwanza 2019.
Mhe. Kwingwa amewataka wazazi kuharakisha zoezi hili la uchangiaji liwe la haraka kwa kujinyima na kujijitoa ili kabla ya Mwezi Machi, 2019 wanafunzi wote wenye alama za ufaulu wawe wameripoti shuleni na kuendelea na masomo ya sekondari ili waweze kutimiza ndoto zao. Aidha; amewataka wazazi kuwa karibu na watoto wao ili katika kipindi hiki cha ukarabati na uboreshaji wa miundombinu ya madarasa kisiwe uchochoro wa kuwatorosha na kuwatumikisha wanafunzi hao katika mashamba, kazi za majumbani na kuwaozesha kwa kisingizio cha kutokuendelea na masomo.
Pia katika kuunga nguvu na amasa ya wananchi Mhe. Kwingwa amechangia mifuko 10 ya saruji ili ikasaidie katika uboreshaji wa miundombinu ambapo kikao kimeridhia kila mzazi mwenye mwanafunzi aliyekosa nafasi kuchangia kiasi chaTsh 30,000 na wananchi wengine watachangia Tsh 20,000 ili kutimiza lengo la mkutano. Mhe. Kwingwa ameitaka Kamati ya watu sita (6) iliyoundwa na wazazi kukusanya michango hiyo kwa ueledi na kusimamia zoezi zima la ukarabati kwa uadilifu wa hali ya juu ili kulinda heshima waliypewa na wananchi.
Akizumgumza kwa niaba ya wananchi Mhe. Amatusi Ilumba (Diwani Kata ya Urambo Mjini) amewapongeza wananchi wa kata zote tatu kwa kuwa na mtazamo chanya na mwamuko wa kuchangia maendeleo katika elimu. Mhe. Lihumba alisema shule ya Ukombozi inatumia majengo yaliyokuwa ya chuo cha uwalimu na kuna mabweni ya zamani ambayo yamechakaa na hayatumiki hivyo yakikarabatiwa yanaweza kutoa vyumba 6 vya madarasa hivyo kuweza kutumika kwa watoto 387 ambao hawakuchaguliwa. Mhe. Ilumba alimuomba Mkuu wa wilaya ya Urambo Bi. Angelina Kwinga kutumia nafasi hii adimu aliyonayo kama mkuu wa wilaya ya Urambo kuzishawishi kata nyinginezo kufanya jitahada za kuchangia ujenzi wa miundombinu kwani bado watabaki zaidi ya watoto 1005 ambao wana alama za ufaulu lakini hawakuchaguliwa awamu ya kwanza.
Alkathalika Ndg Nassibu Daudi Mkazi wa Urambo Kati katika kuunga mkono hoja ya uchangiaji ukarabati wa miundombinu ya madarasa alishukuru uongozi wa kata na mkuu wa wilaya ya Urambo kwa kuandaa mkutano huo kwani matokeo yatawanufaisha watoto wao hivyo akawaomba wazazi wenzake washikamane ili kuhakikisha wanatimiza lengo la kuwasaidaia watoto 387 wanapata elimu ya sekondari. Alimuomba mkuu wa wilaya ya kuwa jambo hili litengenezwe kama sheria kwa kusema " mimi nitegemee mkuu wa wilaya aseme kama rais wa wilaya, alafu lile agizo lako atakayelikiuka aone uo moto wa mkuu wa wilaya" alisitiza Ndg Daudi.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.