Leo ni siku ya wafanyakazi Duniani na hapa kwetu Tanzania imezoleeka kama siku ya Meimosi ambayo huazimishwa kila tarehe 01.05 ya kila mwaka. Kitaifa sherehe za sikukuu hii zimehazimishwa uko Sokoine-Mbeya na kuhutubiwa na mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Rais wa Jamhurim ya Muungano wa Tanzania. Watumishi wa Urambo wakiwemo wa sekta binafsi na serikali katika kuazimisha siku ya leo ya Meimosi wamekutana katika viwanja vya Mwananchi Square vilivyopo katikati ya mji wa Urambo ili kusherekea sikuu yao kama ilivyozoeleka. Awali watumishi hao walianza kwa maandamano yaliyoanzia makao makuu ya wilaya ya Urambo kisha kuzunguka barabara na mitaa kadhaa ya wilayani huku wakiimba nyimbo mbalimbali, wakipiga matarumbeta, ngoma, vigelegele na shangwe ili kuchagiza shamrashara za sherehe ya sikuu hii ya leo tarehe 01.05.2019.
Pamoja na kuwepo kwa kwaya, michezo ya ngoma na usomaji wa lisara kama ilivyozoeleka kwa lengo la kuitaka serikali kuwajali watumishi wa umma kwa masilahi na stahiki zao mbalimbali, pia watumishi hao wa sekta zote walipata nafasi ya kuonyesha bidhaa/huduma kwa Katibu Tawala(W)-Kaliua Ndg Michael Saimon Nyahinga kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Urambo ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi wa sherehe hizo.
Akitembelea mabanda hayo ya taasisi mbalimbali Ndg Nyahinga alipata fursa ya kuelezwa kujionea baadhi ya huduma na bidhaa zinazotolewa kwa wananchi wa Urambo kama ifuatavyo:-
Katika banda la Mahakama, Hakimu Mkazi wa Urambo Ndg Onesmo I. Nicademo amemweleza mgeni rasmi Ndg Nyahinga juu ya uwepo wa dawati la kuwashauri wananchi juu ya mambo ya kisheria na upatikanaji wa haki kupitia Mahakama ili kuhakikisha wananchi wa Urambo wanapata haki zao kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuuri ya Muungano wa Tanzania. Mgeni rasmi alipongeza idara ya Mahakama na kuwataka wananchi wenye migogoro na mashauri katika hatua mbalimbali kutumia mwanya huo wa kipekee kupitia dawati hilo.
|
Katika banda la TAKUKURU Afisa Uchunguzi Ndg Oscar Chingilile amemweleza mgeni rasmi kuhusu uwepo wa baadhi ya watumishi wa sekta binafsi na wa umma ambao hawana maadili wamekuwa na tabia ya kujihusisha na vitendo vya rushwa iwe wakati wa kutoa ajira, huduma ama kudai stahiki zao. Ndg Chingilile amesema kuwa TAKUKURU-Urambo inaendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali kupitia semina, mikutano ya hadhara na vipeperushi kila wanapopata nafasi ili kuwafikia watu wote lengo kuu ikiwa ni kutokomea rushwa wilayani Urambo.
|
Banda la Idara ya Afya, katika banda hili liligawanywa katika sehemu za TOHARA ya wanaume, Upimaji wa VVU/UKIMWI na Utoaji wa DAMU SALAMA. Sehemu ya TOHARA kwa Wanaume Mtoa Huduma wa Jamii Ndg Joram Chay amemweleza mgeni rasmi ya kuwa huduma hii ya TOHARA kwa wanaume inapatikana katika Hospitali ya wilaya ya Urambo kwa siku 7 na katika muda wa kazi yaani saa 1:30 Asubuhu hadi saa 9:30, na alieleza huduma hii inatolewa bure hivyo wananchi wafike ili wapate huduma hii na kufikia 01.05.2019 wanaume 590 wamenufaika na huduma hii.
Sehemu ya kupima VVU/UKIMWI Tabibu Daraja la I Ndug Charles Kulebelwa amemweleza mgeni mgeni rasmi kuwepo huduma hii ya bure ya kupima VVU/UKIMWI katika Hospitali ya wilaya ya Urambo na ushauri utolewa kwa wale wanakutwa wameambukizwa ili wajua namna ya kuishi kwa matumani.
|
Sehemu ya DAMU SALAMU, Mganga Mkuu wa Afya Ndg Paul Swakala ameeleza ya kuwa Hospitali ya wilaya ya Urambo inatekeleza zoezi la upatikana wa damu salama kwa ajili ya kunusuru vifo vya mama na mtoto, ameeleza kupungua kwa vifo vya mama na mtoto kutoka 25 mwaka 2015 hadi kufikia kifo 3 mwaka 2018 hadi tarehe.01.05.2019 kuna kifo 1 tu pia Ndg Swakala amesema lengo la Hospitali ni kuwa na kifo 0 cha mama na mtoto. Mgeni rasmi alifurahishwa na huduma zote tatu muhimu kwani lengo lake ni kufanya wananchi na watumishi wa urambo wawe na afya nzuri ili waweze kuzalisha na kutimiza majukumu yao kama kawaida. Amewaasa wanaume kuchangamkia fursa hii adimu ya TOHORA na kuwaomba wananchi na watumishi wote kujenga tabia ya kupima afya zao na si kutembea wakia gizani bila ya kutojua maradhi waliyonayo. Aidha amewataka wataalamu wa Idara ya Afya kuendelea kutoa elimu ya kuchangia DAMU SALAMA ili kutokomeza kabisa vifo vya Mama na Mtoto vitokanavyo va ukosevu wa damu na kuondoa imani potovu kwa jamii ya kuwa ukichangia damu unapatwa na matatizo mbalimbali.
|
Katika banda la benki ya NMB Afisa Mahusiano Ndg Jacob Laurian alimweleza mgeni rasmi juu ya huduma/bidhaa zinazotolewa na benki ya NMB kuwa ni pamoja na huduma ya Salary Advance kwa kukopa mshahara wako kwa simu huduma inayoongeza usiri kwa watumishi kwani huduma hii imesaidaia watumishi kuondokana na kadhia ya kukopakopa mitaani kwa masharti ya kuweka thamani za nyumbani au kuacha kadi ya benki kipindi ambacho mshahara unakua haujatoka. Sanjali na ilo Benki ya Nmb pia imeboresha huduma zake za mikopo kwa watumishi uku ikiwaruhusu kukopa adi 65% ya mishahara yao na riba ikiwa imepunguzwa adi 17% uku pia ikinunua mikopo toka taasisi mbali mbali za kifedha walipokopa watumishi ikiwemo Bodi ya mikopo. Sambamba na ilo ameeleza kuwa Benki ya NMB imetoa ajira zaidi ya 11 kwa wananchi wa Urambo na viunga vyake kwa kuwapa uwakala wa NMB hivyo kurahisisha hupatikanaji wa huduma za kibenki maeneo mengi wilayani Urambo.
|
Katika banda la benki ya CRDB Miss Deborah Lwekamwa Meneja Biashara tawi la Urambo alimweleza mgeni rasmi kuwa benki ya CRDB imepiga hatua kubwa kwa kuazisha BIMA za aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na Bima ya Maisha,Afya, Vyombo vya Moto, Nyumba na uwepo wa akaunti maalamu kwa akina mama ijulikanayo kama Malkia Akaunti, akaunti ya Fahari isiyokuwa na gharama za uendeshaji mahusuhi kwa ajili ya wajasiliamali wadogo, akaunti ya Junior Jumbo maarufu kama JJ kwa ajili ya watoto, huduma za sim akaunti ambapo simu ya mteja ndio akaunti yake na kumuwezesha kujiwekea akiba pamoja na uwezo wa kufungua kikundi chenye watu zaidi ya watano mpaka watu mia tatu, mikopo kwa vikundi vya Bodaboda na wajasiliamali lengo ikiwa ni kuwainua akina mama na vijana kiuchumi.
|
Mikopo kwa ajili ya watumishi ambapo riba imeshuka mpaka kufikia asilimia 16 pamoja na mikopo ya wafanyabiashara mbalimbali.Pia Miss Deborah alimueleza mgeni rasmi juu ya huduma ya Fahari Huduma Wakala ambapo wateja na wasio wateja wa benki wanaweza kupata huduma zote za kibenki kupitia mawakala wetu wanaopatikana sehemu mbali mbali mijini na vijijini. Miss Deborah alimkaribisha mgeni rasmi pamoja na watumishi wote kufika benki ya CRDB tawi la Urambo kwa ajili ya kujipatia huduma hizo na nyinginezo lukuki zinazotolewa na benki ya CRDB.
Ndg Nyahinga alipongeza huduma zote zinazotolewa na Benki zote mbili na kuwasihi wananchi na watumishi wa Urambo kuchangamkia fursa hizo.
Katika banda la kampuni ya simu ya mawasiliano ya tiGo, Msimamizi Mkuu wa Duka la tiGo Ndg Godian Mkomagi ameeleza bidhaa na huduma bora zinapatikana wilayani Urambo kutoka kampuni ya tiGo ikiwemo simu za kisasa kwa bei nzuri, kutoa ajira kwa wakala wa tiGoPesa 60 apa wilaya Urambo hivyo kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za tiGo kwa wananchi. Mgeni rasmi amewashukuru sana kampuni ya tiGo kwa ushirikiano wao na kuwaomba kupanua huduma ya mawailiano kwa kujenga minara kuongeza kasi ya mawasiliano maeneo ya pembezoni mwa wilaya ya Urambo hali ya mawasiliano ya simu ni duni.
|
Katika Banda la TRA Afisa Mwandamizi wa Elimu na Huduma mkoa wa Tabora Ndg Geofrey Conoro ameelezea kwa mgeni rasmi huduma zinazotolewa na TRA -Urambo ikiwa ni pamoja na elimu ya kodi kwa wafanyabiashara na watumishi, matumizi ya mshine za EFD na kutoa TIN namba kwa wananchi wote wenye kitambulisho cha Taifa-NIDA na ulipaji wa kodi ya majengo.
|
Akihutubia umati wa watumishi na wananchi kadhaa waliofika katika viwanja vya Mwananchi Square Ndg Nyahinga amepongeza wafanyakazi wa sekta zote kwa kuhenzi kauli ya 'APA KAZI TU" kwa utoaji wa huduma bora na nzuri kwa wananchi wa Urambo na kuwasihi kuongeza hali ya kujituma zaidi na kuvuta subila kwani Serikali inaendelea na uboresheshaji wa stahiki na maslai yao.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.