1. UTANGULIZI
Wilaya ya Urambo ina jumla ya hekta 87,984 zinazofaa kwa kilimo, kati ya hizo hekta 10,400 zinafaa kwa kilimo cha Umwagiliaji ,eneo hili ni sawa na 11.8% ya eneo linalofaa kwa kilimo. Wilaya ina skimu moja inayotekeleza kilimo cha umwagiliaji.Kilimo katika Wilaya ya Urambo kinategemea mvua kwa sehemu kubwa.
2. UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMWAGILIAJI USSOKE MLIMANI
Mradi wa Ussoke Mlimani upo katika Tarafa ya Ussoke, kata ya Uyumbu na unatekelezwa na vijiji vya Ussoke Mlimani na Yela Yela. Malengo makuu ya mradi ni kuchangia katika kuwezesha kufikia lengo la usalama wa chakula (kwa Kaya,na Taifa) kwa kuongeza uzalishaji wa chakula kupitia skimu za umwagiliaji zilizo jengwa au kuendelezwa vizuri. Vile vile kuongeza kipato kwa jamii ili kuwezesha kuondoa au kupunguza umaskini kwenye jamii.
Mradi ulianza kutekelezwa mwaka 2009/2010 kwa kufanya tafiti mbali mbali za upimaji wa sura ya ardhi,usanifu, upimaji udongo na utafiti wa athari za mazingira. Kazi za ujenzi wa bwawa zilianza kutekelezwa msimu wa 2011/2012. Kampuni ya Lead Com and Amp JV ya Box 7240 Dar es salaamu ilitekeleza kazi za ujenzi wa bwawa kwa gharama ya shilingi 326,526,565.00.Bwawa lina uwezo wa kuvuna maji ya mvua ya ujazo wa mita 849,890.63 (849,890.63 m3) zenye uwezo wa kumwagilia jumla ya hekta 211 sawa na ekari 527.5 za mpunga. Eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji katika eneo hili ni hekta 554 (1,385 ekari).Mradi kwa sasa unaendeleza hekta 122 (ekari 305).
Msimu wa 2012/2013 kuanzia tarehe 01.12.2012, kampuni ya Geocon Company limited ya Box 6354 Dar es Salaam ilianza kujenga baadhi ya miundo mbinu ya umwagiliaji kwa gharama ya shilingi 177,011,480.00 na kukamilisha 24.04.2013.
Mwaka wa fedha wa 2015/2016 tarehe 20.06.2016, Halmashauri ilipokea fedha za kuendeleza mradi wa Ussoke Mlimani jumla ya shilingi 331,000,000.00 kutoka mfuko wa SSIDP. Fedha zote zilihamishiwa kwenye akaunti ya walengwa ya Umoja wa Watumiaji maji ya Umwagiliaji Ussoke Mlimani/Yela Yela (UMWAMUUYE).Umoja huu una wanachama 239 kati yao wanawake 117 na wanaume 122.
2.1 UTEKELEZAJI MRADI KWA KUTUMIA FEDHA ZA SSIDP
Fedha za utekelezaji wa mradi zimeanza kutumika mwaka wa fedha 2016/2017 baada ya kukamilisha taratibu za zabuni za kumpata mkandarasi.Kampuni ya M & A Engineering ltd. and Manguto investment co. ltd. (JV) ya S. L. P. 1182, Shinyanga imesaini mkataba namba LGA/122/2016 /2017/W/20 tarehe 25.10.2016 na kuanza kazi 03.11.2016. Kazi itakazotekelezwa kwenye mkataba ni za shilingi 321,870,627.24 ( Pamoja na VAT). Mkandarasi ameishakamilisha kazi zilizoainishwa kwenye mkataba.Jedwali Na.1 linaonyesha miundo mbinu iliyotekelezwa katika skimu.
Table 1: MIUNDO MBINU ILIYOKAMILIKA SKIMU YA USSOKE MLIMANI
SN
|
MIUNDOMBINU ILIYOPO
|
KIASI
|
KIZIO
|
MAELEZO
|
||
1
|
Mfereji mkuu uliojengwa kwa mawe (MC)
|
175
|
m
|
|
||
2
|
Mfereji mkuu wa kati Namba 1, uliojengwa kwa mawe (SC1)
|
1350
|
m
|
|
||
3
|
Mfereji mkuu wa kati Namba 2, uliojengwa kwa mawe (SC2)
|
878
|
m
|
|
||
4
|
Mifereji 3 ya mashambani (TCs) upande wa SC1
|
345
|
m
|
|
||
5
|
Mifereji 4 ya mashambani (TCs) upande wa SC2
|
742
|
m
|
|
||
6
|
Mitaro 2 ya pembeni (CD) pembeni mwa barabara ya SC1 na SC2
|
2115
|
m
|
|
||
7
|
Mitaro 2 ya pembeni (CD) karibu na bwawa
|
264
|
m
|
|
||
8
|
Barabara 2 za huduma (SR) pembeni mwa, SC1 na SC2
|
2035
|
m
|
|
||
9
|
Vigawa maji (DB) kwenye SC1 kila inapounganika na TC
|
11
|
No.
|
|
||
10
|
Vigawa maji (DB) kwenye TC1/SC1
|
2
|
|
|
||
11
|
Vigawa maji (DB) kwenye SC2 kila inapounganika na TC
|
9
|
No.
|
|
||
12
|
Daraja la mfereji (Flume), kwenye SC1
|
1
|
No.
|
|
||
13
|
Punguza kasi (Drop) kwenye SC1
|
2
|
No.
|
|
||
14
|
Punguza kasi (Drop) kwenye baadhi ya TCs
|
13
|
No.
|
|
||
15
|
Daraja mbonyeo (Drift) kwenye barabara pembeni mwa SC1
|
1
|
No.
|
|
||
16
|
Njia ya maji kwenye mfereji SC1 (Cross Drainage)
|
1
|
No.
|
|
||
17
|
Vivuko vya wanyamakazi
|
2
|
No.
|
|
||
18
|
Vivuko kwenye DB
|
14
|
No.
|
|
||
19
|
Mageti ya chuma DB ya SC1na SC2.
|
2
|
No.
|
|
||
20
|
Tupio la maji (Spillway)
|
1
|
No.
|
|
||
21
|
Bwawa na miundominu yake ya kufungulia maji
|
1
|
No.
|
|
Kibanio cha Maji | Mtaro wa Kutilisha Maji Shambai | Shamba linapokea Maji ya Mradi |
3. MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WA MRADI NA WAKULIMA
Kamati ya ujenzi wa mradi imejengewa uwezo wa kusimamia mradi kupitia mafunzo ya usimamizi wa ujenzi sambamba na mafuzo ya usalama wakati wa ujenzi ambayo yalitolewa na Halmashuri ya wilaya ya Urambo ikishirikiana na mradi wa TANCAID II. Pia wakulima wameshapata mafunzo ya kilimo bora cha mpunga kupitia shamba darasa lililolimwa msimu 2015/2016 na kuvuna gunia 27 kwa ekari ukilinganisha na mavuno ya wakulima kwenye ekari ni gunia 10-15. Mradi una lengo la kuboresha uzalishaji wa mpunga kutoka uzalishaji wa tani 02 kwa hekta hadi tani 06. Wakulima 50 wameshiriki kulima mashamba yao msimu 2015/2016.Msimu huu 2016/2017 wakulima wa skimu wameuziwa mbolea ya ruzuku aina ya Urea jumla ya mifuko 60 ili kuboresha kilimo chao cha mpunga.
4. CHANGAMOTO NA UTATUZI WAKE
Changamoto iliyojitokeza ni mvua zilizokuwa zinanyesha zilipunguza kasi ya ujenzi.Mkandarasi aliomba kuongezewa muda na akakubaliwa kwa kuongezewa muda wa siku 30 ambazo zitakamilika tarehe 01.05.2017.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.