Mkuu wa Wilaya ya Urambo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi (SACC)Elibariki Bajuta amewataka waendesha Pikiki maarufu Bodaboda Wilayani Urambo kuheshimu vyombo vya Ulinzi na Usalama na kushirikiana navyo ili kutokomeza Ajali za barabarani. SACC Elibariki Bajuta amesema hayo wakati alipokutana amekutana na waendesha pikipiki za abiria maarufu kama Bodaboda tarehe 27.05.2024 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo. SACC. Bajuta amekutana na waendesha pikipiki hao ili kujadili masuala mbalimbali yanayowagusa madereva hao na vijana wa Urambo kwa ujumla. Aidha Mkuu wa Wilaya alifanya mkutano huo akishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bi. Grace Quintine pamoja na baadhi ya wakuu wa idara za Ulinzi na Usalama Wilayani Urambo. Hata hivyo SACC Bajuta alisisitiza Bodaboda kuwa na Uongozi halali unaotambulika na kusajiliwa ili kusaidia Bodaboda kuweza kupata fursa mbali mbali kama Mikopo.
Aidha katika kuhakikisha Hilo linatimia, SACC. Bajuta alihakikisha uchaguzi unafanyika na kupatikana kwa Viongozi wa Umoja wa Bodaboda Wilaya ya Urambo.
Viongozi waliochaguliwa ni:
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bi Grace Quintine amesema kuwa Bodaboda wanaweza kupata mikopo ambayo itaweza kuwainua kiuchumi na kuwasaidia kiuchumi. Hata hivyo Bi.Grace amesema Mikopo na fursa nyinginezo, zitapatikana pale ambapo Bodaboda watasajiliwa na kutambulika. Sambamba na hilo OCD wa Wilaya ya Urambo amesisitiza Bodaboda kutii sheria za barabarani na kuvaa kofia ngumu zenye kioo na nguo nzito ili kulinda afya zao. Aidha DTO Bi. Mshaka alipata wasaa wa kutoa utaratibu wa kufuata ili kupata leseni, na kueleza kuwa kwa sasa unaandaliwa utaratibu mzuri ambao utawezesha Bodaboda Urambo kupata mafunzo pamoja na leseni. Pia amewataka Bodaboda kuendesha vyombo vya moto vilivyosajiliwa ili kuepusha kukamatwa kama Mhalifu wa pikipiki iliyoibiwa.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Urambo SACC. Bajuta pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, wameahidi kushirikiana na Bodaboda katika matukio mbalimbali.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.