Katibu Tawala wa Wilaya ya Urambo Ndg Paschael Byemelwa amewatoa hofu wananchi wa wilaya ya Urambo juu ya upatokanaji wa vitambulisho vya Taifa-NIDA wakati akihutubia Baraza la wahe. Madiwani la uwasilishaji wa taarifa za kata tarehe 29.04.2019, katika ukumbi wa Halamashauri wilayani Urambo.
Akitoa ufafanuzi juu ya zoezi linaloendelea la ugawaji na uandikishaji wa wananchi wilayani Urambo, Ndg Byemelwa aliwaeleza wahe. Madiwani kutambua ya kuwa kila mkazi mwenyesifa aliejiandikisha atapata kitambulisho cha Taifa-NIDA kwani zoezi la ugawaji na usambaji wa vitambusho hivyo linaendelea kwa kusimamiwa na maafisa wa NIDA walioko apa wilayani Urambo.
Ndg Byemelwa amewasihi wahe. Madiwani na watendaji wa kata kila mmoja kwa nafasi yake kuwatoa hofu wananchi katika ngazi za vitongoji, vijiji na kata hasa kipindi hiki tunapoelekea katika usajili wa laini za simu za mawasiliano kwa kutumia alama za vidole yakuwa na imani na ofisi za NIDA kwani vitambulisho vinaendelea kutolewa pamoja na kuwepo kwa changamoto za hapa na pale.
Ndg Byemelewa alisema "zoezi hili la uandikishaji na utoaji wa vitambulisho linahitaji umakini sana ili kuhakikisha kitambulisho kinatolewa kwa raia wa Tanzania tu kwani kitatumika kama Kitambulisho cha Uraia au Taifa na matumizi mengine mbalimbali yenye tija na maslahi kwa Taifa, na kuhusu usajili wa laini za simu za mawasiliano tayari Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amelitolea ufafanuzi hivyo halihitaji tena mjadala mrefu" alilisitiza Ndg Byemelwa.
Aidha, Ndg Byemelwa amepongeza ushirikiano baina ya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Urambo wakati wa ugawaji wa jumla ya vitambulisho 8125 vya wajasiliamali wadogo ilivyopokea kama mgao wa wilaya na tayari vitambulisho hivyo vyote vimetolewa kwa wajasiriamali wadogowadogo na kiasi cha Tsh 162,500,000/= (Milioni Miamoja Sitini na Mbili na Laki Tano) zilipatikana na zimepelekwa benki. Akitoa shukrani za pekee kwa Kitengo cha Biashara na kwa watendaji wa Kata na Vijiji, Ndg Byemelwa alieleza kuwa zoezi la ugawaji wa vitambuisho limefanikiwa kwa asilimia 100 kwani hakuna kitambulisho ata kimojo kilichopotea wala kiasi cha fedha ambacho hakikupelekwa benki.
Alkadhalika Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Urambo Ndg Adamu Malunkwi alimpongeza Katibu Tawala(W) Urambo kwa ufafanuzi mzuri na wa kina wa upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa-NIDA kwa kuwa amewaondolea wahe. Madiwani sintofahamu iliyokuwepo na kuhaidi watawajulisha wananchi ili wawe na subira katika hilo. Pia Mhe. Malunkwi akionyesha uso wenye furaha na bashasha alipongeza mafanikio, ushirikiano na mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji(W)-Urambo kwani yamechangia kasi ya ukamilishaji wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya wajasiliamali kwa wakati; alisema vitambulisho hivyo vitawasidiwa wajasiliamali wa Urambo kufanya biashara zao kwa amani, utulivu na kuondokana na kero za kudaiwa ushuru kama ilivyokuwa awali.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.