Na Edward C Rumanyika
Kikao cha kwanza mwaka 2021 cha Wadau wa Elimu kimefanyika leo 10 Jumatano, 2021 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Urambo lengo kuu ikiwa ni kujadili changamoto za elimu wilayani Urambo
Katika hali hisiyotarajiwa na ya kushangaza, wadau wa Elimu Urambo wamehuzunishwa na taarifa ya mwitikio mdogo kwa wana Urambo wa kuchangamkia na kutumia fursa za elimu zinazopatikana na zinazotolewa bure katika vyuo vya VETA-URAMBO na FDC-URAMBO.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti; wakuu wa vyuo hivyo wameeleza kuwepo kwa nafasi za wanafunzi 58 ufadhili wa Mhe. Magret Simwanza Sitta(MB) Jimbo la Urambo katika chuo cha VETA-URAMBO na ufadhili wa Mfuko wa Kukuza Ujuzi (Skill Development Fund-SDF) chini ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika mradi wa Uchomeleaji na Uungaji wa vyuma bure katika chuo cha FDC-URAMBO lakini kwa wilaya ya Urambo ni wanafunzi 8 tu waliojitokeza kujiunga na VETA-URAMBO na 15 kujiunga na FDC-URAMBO ingali gharama za masomo ni bure hali iliyowashangaza Wadau wa Elimu.
Akiongoza kikao hicho cha Wadau wa Elimu kutoka kila tasnia ndani ya wilaya ya Urambo , Katibu Tawala(W) Ndg. Paschael Byemelwa aliwasilisha changamoto zinazoikabili sekta ya elimu na kutoa fulsa kwa wadau wa elimu kujadili, kuchangia na kupendekeza afua za utekelezaji wakati wa utatuzi wa hizo changamoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Urambo. "Kila mmoja wetu ajipime kulingana na hizi changamoto katika mazingira ulipotoka, na apa tuko darasani kujifunza ili mwisho wa kikao hiki kila mmoja wetu aondoke na kitu ulichojifunza au cha kuiga kupitia darasa hili" alizungumza Ndg Byemelwa.
Awali kaimu Afisa Elimu Msingi Ndg. Gambalala Suga na Afisa Elimu Sekondari Bi Sara Nalogwa waliwasilisha taarifa za ufaulu wa mtihani wa upimaji wa darasa nne na kidato cha pili, 2020 na mtihani wa Taifa wa darasa la saba, kidato cha nne na sita, 2020 na kusisitiza kuwepo kwa shule zinazofanya vizuri katika mitihani ya kila mwaka na nyingine ufaulu wake siyo wa kuridhisha .
Aidha Mwenyekiti wa kikao cha wadau wa Elimu Ndg Byemelwa, ametoa zawadi na pongezi kwa shule zilizofanya vizuri kwa mitihani ya mwaka 2020 na kutoa zawadi ya bendera nyeusi kwa shule zenye ufaulu usioridhisha ili ikawe chachu ya kupambana kuhakikisha wanafia kiwango cha ufaulishaji wa asilimia 80%.
Akihitimisha kikao hicho Ndg Byemelewa amewapongeza wadau wa Elimu Urambo kwa mawazo na yao azuri na yenye tija katika kuhakikisha changamoto zilizo ndani ya uwezo wao zinapatiwa ufumbuzi ili kuweka mazingira rafiki ya upatikanaji wa elimu kwa kizazi cha leo na kijacho ndani ya wilaya ya Urambo. Na pia amewataka wadau wa Elimu Urambo kupeleka ujumbe ngazi ya vijiji na kata wa fursa za ufadhili zilizipo katika vyuo vya VETA-URAMBO na FDC-URAMBO ili jamii inufaike na uwepo wa fursa hizo.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.