Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ametoa Hati 103 za umiliki wa ardhi za kimila ambazo hazina kikomo kwa wakazi wa Kijiji cha Itebulunda kata ya Nsenda wakati wa mkutano mkuu maalumu wa kijiji ulifanyika katika viwanja vya ofisi ya kijiji cha Itebulanda kata ya Nsenda Mei 28,2018. Hadi kufikia Juni 10, 2018 jumla ya hati 2000 za umiliki wa ardhi zisizokuwa na ukomo zinatalajiwa kutolewa kwa wananchi wakazi wa kijiji cha Itebulanda.
Akizungumza na wananchi wa Itebulanda, amewaeleza umuhimu wa kuwa na hati hizo za kimila zisizo kuwa na ukomo wa umiliki wa ardhi na faida zake ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani ya ardhi, kuwaongezea fursa ya kukopa kwa kuwa hati hizo zinatambulika katika taasisi mbalimbali ikiwemo benki, na uwezekano wa kubadilisha ardhi na vitu vingine vya thamani.
Amewasihi kutumia muda mchache uliosalia kuhakikisha wanautumia vizuri kwa kukamilisha taratibu zote za umilikishwaji wa ardhi kwa kuwapatia taarifa muhimu wataalamu wa zoezi hilo. "Itebulanda amkeni na karibu Duniani, tambueni thamani ya ardhi mliyoikalia kwa kupima na kupatiwa hati ya ardhi yenu. Mwenye maskio na askie" alisema mkuu wa mkoa wa Tabora.
Awali akitoa taarifa ya zoezi hilo liloanza Mei 02, 2018 Ndg Jobu Kiungo mratibu wa mradi wa MiomboLands kanda ya Magharibi alisema kutokana na umuhimu wa zoezi hilo, ameongeza muda wa siku 10 zaidi kutoka tarhe 30.05.2018 hadi Juni 10, 2018, ili kuhakikisha wakazi wote wa kijiji cha Itebulanda walionyesha nia ya kupewa hati za umiliki wa ardhi wananufaika kwani ni la kipekee na halijawahi tokea, hati za umiliki wa ardhi zisizokuwa na kikomo zaidi ya 1500 kutolewa kwa mkupuo.
Akiongea kwa niaba ya wananchi wakazi wa kijiji cha Itebulanda, Ndg Erasto Mahona ambaye pia ni Mhe. Diwani wa kata ya Nsenda alitoa shukulani za kipekee kwa mradi wa MiomboLands kwa kuwajali na kuwapa kipaumbele cha kuwa wa kwanza katika mkoa wa Tabora na akawasihi wananchi wenzake watumie nafasi hii ya kipekee kuhakikisha wanapatiwa hati miliki za ardhi yao ili kuondokana na migogoro ya mipaka ambayo inaweza jitokeza siku za usoni.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.