Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Robo ya kwanza 2024/2025 umefanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Urambo tarehe 01.11.2024 kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kupokea taarifa kutoka katika kamati mbalimbali za Halmashauri. Aidha katika Mkutano huo Baraza hilo liliazimia na kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha maeneo yote ya Serikali na Taasisi za Umma yanapatiwa hati miliki.
Aidha azimio hilo linatoa nafasi kwa Taasisi nyingine binafsi na watu binafsi kupatiwa hati miliki za maeneo yao kwani faida za kuwa na hati miliki ni nyingi sana. Akizungumza kuhusu suala hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mhe. Adam Malunkwi amesema kuwa faida za kuwa na hati miliki ni nyingi ikiwemo kuweza kupata fursa za wawekezaji mbalimbali kutokana na wawekezaji wengi kuhitaji uhakika wa maeneo wanayokwenda kuwekeza fedha zao.
Akiungana na hoja ya Mwenyekiti wa Halmashauri kuhusu faida za kuwa na hati miliki, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bi. Grace Quintine amesema kuwa ni muhimu sana kuwa na hati miliki hivyo kama Halmashauri imejipanga na tayari imeanza mchakato wa kupima maeneo na utekelezaji wa mpango wa matumizi bora ya ardhi ambao utasaidia kuondoa mauzo na matumizi holela ya maeneo ya ardhi hivyo kupata maeneo kwa ajili ya uwekezaji na ujenzi wa miradi ya maendeleo.
"Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi Jitokeze kushiriki Uchaguzi"
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.