Kamishina Msaidizi Mhe. Elibariki Bajuta Mkuu wa wilaya Urambo akiambatana na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji(W) Urambo na baadhi ya Wataalamu ametembelea na kukagua ujenzi wa Zahanati na shule katika kijiji cha Imamakoye leo Novemba 6, 2023 na kubaini ya kuwepo viashiria vyakutumia fedha za umma bila ya kuzingatia Sheria, kanuni na taratibu.
Mhe. Bajuta ameshangazwa kusikia jumla ya Tsh 90 milioni zimetolewa kwa awamu tatu (milioni 40 mara mbili kisha 10 milioni) na Serikali lakini ujenzi wa zahanati hiyo ulioanza mwaka 2014 hadi leo bado haujakamilika na fedha zaidi imeendelea kutolewa kwenye akauti ya maendeleo ya kata licha ya awali ofisi ya mkuu wa wilaya kuzuia matumizi ya fedha hizo.
Pia Mhe. Bajuta ametembelea mradi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na ofisi ya walimu ambapo mradi umesha gharimu takribani Tsh 7,640,000 na umeanza kujengwa tangu mwaka 2022 lakini hamna Kamati ya Usimamizi katika mradi huo.
Mhe.Bajuta amemwagiza Mkurugenzi Mtedaji(W) Urambo kuhakikisha anajiridhisha na ukubwa wa eneo la ujenzi unaondelea wa shule kama linakidhi vigezo ikiwa ni pamoja na kuongeza miundombinu mingine na ipate sifa za kusajiriwa na Serikali, vinginevyo ujenzi usimamishe haraka iwezekanavyo.
"Mimi napenda nione matokeo ya fedha ya umma imefanya nini, nataka nione zahati inafanya kazi, shule inafanya kazi, hivyo ntoe rahi kwa viongozi wa serikali ya kijiji na kata mliopo hapa, kazi yenu ni kusimamia watendaji hawa wafanye kazi ikiwemo kusimamia miradi ya maendeleo na siyo na nyie mfanye kazi ya kujenga hapo hatutaelewana" amesema Mhe. Bajuta.
Aidha ameagiza ofisi ya TAKUKURU Urambo kufanya ufatiliaji wa haraka na kina kwenye ujenzi wa zahanati na shule ili kubaini kama taratibu za matumizi ya fedha za umma umezingatiwa na kusisitiza ya kuwa atawachulia hatua wale wote watakaobanika walishiriki kwa namna moja au nyingine.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.