Na Edward C Rumanyika-Urambo DC
Naibu waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Andrea Mathew (MB) akiwa ameambatana na wataalamu kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na viongozi wa makampuni ya Mawasiinao ya simu ya Airtel, Halotel, TiGo, TTCL na Vodacom, amefanya ziara ya kutembelea maeneo yenye changamoto za mawasiliano ya simu na redio katika wilaya ya Urambo.
Ziara hiyo iliyofanyika 16 Machi, 2021 Mhandisi Kundo Andrea Mathew aliweza kufanya mkutano wa ndani katika ukumbi wa mkuu wa wilaya ya Urambo na kisha kutembelea maeneo yenye changamoto zaidi ya mawasiliano katika kata za Songambele kijiji cha Mlangale, Kasisi jijiji cha Wema na Uyumbu kijiji cha Nsogolo kwani Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ilitoa ruzuku ya kiasi cha Tsh 117,500,000 kufikisha huduma ya mawasiliano kata ya Kasisi vijiji vya Azimio,Kasisi, Mapambano na Wema ili kutatua changamato ya mawasiliano katika vijiji husika.
Mhe Naibu waziri ameweza kubaini kuwepo kwa janja janja ya baadhi ya makampuni ya simu za mkononi kwenda kinyume na mikataba yao kwa kuchelewesha kuhuisha teknolojia ya huduma ya awali ya mawasiliano (2G) na kwenda kwenye teknolojia ya kisasa ya mawasiliano yenye kasi zaidi (3G/4G) ili kuwafikia wananchi wengi kwa huduma nzuri na bora, licha ya kupokea fedha kutoka Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) za kujenga minara na kuboresha mawasiliano maeneo yasiyo na mvuto wa biashara kwa watoa huduma za mawasiliano wamekuwa wakienda kinyume na mkataba yao.
Kutokana na hali ya udanganyifu uliobanika wakati wa ziara hiyo, Mhe. Mathew ameeleza namna Serikali ya Awamu ya Tano kupitia TCRA imejipanga kuhakikisha inathibiti makampuni ya simu kwa kupima ubora wa huduma ya sauti, ujumbe mfupi na kufikia 2 Aprili, 2021 kutakuwepo na programu ya rununu (mobile App) itakayoratibu matumizi ya vifurushi vya intaneti kupitia simu ya mteja na tayari faini na adhabu zimeanza kutolewa kwa baadhi ya makampuni na TCRA.
Akihutubia wananchi wa kijiji cha Nsogolo kata ya Uyumbu Mhe. Mathew alipongeza ushirikiano wa dhati ulipo kati ya ofisi ya Mkuu wa wilaya, Mbunge wa Jimbo la Urambo na Mkurugenzi Mtendaji katika swala zima la kuwaletea maendeleo wananchi wa Urambo na hakusita kusema hiyo ndiyo chachu ya yeye kuja kujionea hali halisi ya changamoto za mawasiliano wilayani Urambo hasa vijijini.
Aidha aliwapongeza wananchi waliojitokeza na kuelezea kero za changamoto ya mawasiliano ya simu wanayopitia na kuwaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha mpito kwani Serikali ya Awamu ya Tano inafanyia kazi changamoto hizo na kueleza ya kuwa "sasa hivi habari ya vifurushi kuisha muda wake na kupotea sahau maana tumeyataka makampuni yote ya simu kuhakikisha mteja anaweza kuhamisha kifurushi chake kwenda kwa mtu mwingine au ata kuhuisha kifurushi kwa kununua kifurushi kama cha awali na vifurushi vitaungana ili muendelee kufurahia huduma na tutasimia hili" alisisitiza Mhe. Naibu waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Urambo, mkuu wa wilaya ya Urambo, Mhe. Angelina Kwingwa amempongeza Naibu waziri kwa ziara yake katika wilaya ya Urambo na hasa kwa maamuzi yake yenye tija ya kufika vijijini ambako changamoto ya mawasilino ni kubwa na kueleza faida ya ziara hiyo itasaidia wananchi wa Urambo na Taifa kwa ujumla kwa sababu baadhi ya makampuni ya mawasiliano ya simu yalikuwa yanadanganya kutoa huduma ya kisasa yaani 3G/4G kumbe hali bado ni 2G uko vjijini maana hapakuwepo na uthibiti.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.