Mhe. Kenani Kihongosi Mkuu wa Wilaya ya Urambo hii leo 21 Julai, 2023 katika ukumbi mkubwa wa mikutano wa Halmashauri amefanya kikao kazi na Viongozi ngazi ya kata wakiwemo Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji, Watendaji wa Vijiji, Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu kwa lengo la kufahamiana na kuwaomba kumpa ushirikiano kuhakikisha miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika taasisi za umma, ngazi ya kata na vijiji inasimamiwa kwa ubora ili iendane na thamani ya fedha inayotolewa na Serikali.
Mhe. Kihongosi amewasihi Viongozi hao kufanya kazi kama timu, kwa ushirikiano na kuacha ujanjaujanja wa kutafuta liziki kupitia hela ya miradi inayoelekezwa katika maeneo yao. "Ndugu viongozi mmeaminiwa na Serikali, nimewaiteni hapa na kuwaeleza haya maana sitaki ugomvi na nyie, lakini tutagomba ikiwa hela ya mradi inayoletwa na Mhe. Dkt. Samia Suluh Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itatumika vinginevyo" Amesema Mhe. Kihongosi.
Mhe. Kihongosi amesisitiza swala la uzalendo kwa Viongozi hao hasa kujituma na kufanya kazi kwa bidii bila kutanguliza maslahi ili wakawe mfano bora kwa watu wanaowaogoza na jamii kwa jumla na watambue watakumbukwa kwa kizazi cha leo na cha kesho kupitia uimara wa miradi hiyo. Pia amewashauri Viongozi hao kutambua ya kuwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya iko wazi wakati wote kufika na kutoa taarifa mapema ikiwa watakutana na changamoto na hata kuomba ushauri vinginevyo akikutwa na dosari atawajibishwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za Serikali.
Aidha, Mhe. Kihongozi amewaomba viongozi hao kushawishi wazazi na walezi kuhakikisha wanachangia chakula ili wanafunzi ngazi ya awali, msingi na sekondari wapate chakula shuleni kwa lengo la kuongeza ufaulu na kupunguza utoro.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2024 Urambo . All rights reserved.