Matukio katika Picha kwenye Maadhimisho ya Miaka 61 ya Muungano wa Tanzania (Tanganyika na Zanzibar) Wilayani Urambo leo tarehe 26.04.2025.
Wilaya ya Urambo tumeadhimisha Siku hii muhimu kwa kufanya matukio ya kijamii, ambapo tumefanya matembezi ya Mshikamano kuanzia yalipo Makao Makuu ya Wilaya hadi hospitali ya Wilaya kupitia katikati ya mji wa Urambo. Aidha tumeweza kufanya Usafi, kupanda miti, pamoja na zoezi la uchangiaji damu salama wa hiari katika Hospitali yetu ya Wilaya.
Sambamba na matukio ya kijamii, tumesikiliza ujumbe muhimu wa Muungano kutoka kwa Mgeni Rasmi wa Maadhimisho haya ngazi ya Wilaya ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Dkt. Khamis Mkanachi.
Aidha tumeungana makundi mbalimbali katika maadhimisho haya ambayo ni Viongozi wa Serikali, Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Urambo, Watumishi wa Serikali, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Urambo jogging Club, Wanawake na Samia, Wananchi wa Urambo, Wanafunzi kutoka baadhi ya Shule za Sekondari na Shule za Msingi Wilaya ya Urambo n.k
Wilaya ya Urambo tunaungana na Watanzania wote kuuombea Kheri na kuahidi kuutunza na kuulinda Muungano wa Tanzania ili Tunu hii iweze kudumu na kurithishwa kwa vizazi vijavyo.
"Muungano wetu ni Dhamana, Heshima na Tunu ya Taifa, Shiriki Uchaguzi Mkuu mwaka 2025"
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.