Baada ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 27.11.2024 kutamatika na washindi wa nafasi mbalimbali kupatikana, hatimaye viongozi hao waliopatikana wameapishwa tarehe 29.11.2024 kwa ajili ya kuanza kutumikia Wananchi waliowachagua. Zoezi la Uapisho limefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Margareth Sitta ambapo Viongozi hao wa Serikali za Vijiji na Vitongoji,Mitaa wamekula kiapo mbele ya Hakimu Mhe. Josephita Zenas Batondana pamoja na Mhe. Rehema Pantaleo Bilikundi.
Katika uapisho huo, viongozi hao wa Serikali za vijiji na vitongoji wameeleza kuwa watakwenda kushirikiana bila kujali vyama vya siasa, dini wala kabila katika kuhakikisha maendeleo yanawafikia Wananchi. Aidha viongozi walioshinda wametokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Civic United Front (CUF) pamoja na Alliance for Change and Transparency (ACT WAZALENDO).
Ikumbukwe kuwa tarehe 27.11.2024 ulifanyika uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa ajili ya kuwapata viongozi mbalimbali ambapo nafasi 59 ni za Wenyeviti wa vijiji, 256 ni Wenyeviti wa Vitongoji, 470 Viti maalumu na 700 ni wajumbe wa Halmashauri za vijiji.
Kazi iendelee
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.