Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bi. Grace Quintine ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo amesema vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu vina haki sawa ya kushiriki Uchaguzi wa Serikali za 2024 kama ambavyo Demokrasia inavyoelekeza kulingana na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Bi. Quintine ameyasema hayo wakati alipokutana Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ofisni kwake wakiongozwa na Bi. Christina Godfrey Mkugwa ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Urambo. Kikao hicho kimefanyika tarehe 01.11.2024 katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kwa ajili ja kujadili kwa pamoja juu ya kanuni na muenendo wa zoezi la Uchukuaji na Urejeshaji wa fomu za kugombea nafasi za uongozi wa Serikali za Mitaa ambapo zoezi hilo limetamatika rasmi tarehe 01.11.2024.
Aidha katika kikao hicho Bi. Quintine amewaeleza viongozi hao kuwa vyama vyote vina haki sawa katika uchaguzi huu hivyo wasisite kutoa mapendekezo na ushauri juu ya zoezi la uchaguzi kwani atahakikisha anatimiza wajibu wake na vyama vyote vinapata haki sawa. Hata hivyo amesisitiza kuwa anayetoa maelekezo yote kuhusiana na uchaguzi Jimbo la Urambo ni Msimamizi wa uchaguzi na siyo mtu mwingine yeyote, hivyo katika uchaguzi huu kila chama kitashiriki sawa na mwenye haki ya kushinda atashinda tu.
Aidha Viongozi hao wa CHADEMA wamemshukuru na kumpongeza Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Urambo kwa maridhiano, utayari wa kuwasikiliza pamoja na ushirikiano anaoutoa kwa vyama vya siasa ili kuhakikisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Jimbo la Urambo unaenda vyema na vyama vinapata haki na kujiona sawa.
Ikumbukwe kuwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 unatarajia kufanyika tarehe 27.11.2024 hivyo ni haki ya kila Mtanzania mwenye sifa kushiriki katika kumchagua kiongozi atakayemletea maendeleo ya Kitongoji, Kijiji au Mtaa.
"Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi"
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.